pmbet

Afrika yawa kimbilio kisa machafuko Mashariki ya kati

Sisti Herman

March 3, 2026
Share :

 

Baadhi ya makampuni makubwa ya usafirishaji duniani yameanza kuelekeza meli zao kupita barani Afrika kufuatia kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mashambulizi yanayohusisha Marekani, Israel na Iran kuongeza hatari za kiusalama katika njia muhimu za baharini.

Makampuni ya kimataifa kama Maersk, Hapag Lloyd na CMA CGM yamesitisha safari kupitia Mfereji wa Suez na eneo la Bab el-Mandeb.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya meli sasa zinalazimika kuzunguka kupitia pwani za Afrika, hatua inayoweza kuongeza umuhimu wa bara hilo katika usafirishaji na biashara ya kimataifa. Wataalamu wanasema mabadiliko hayo yanaweza kufungua fursa mpya za kiuchumi kwa nchi za Afrika zinazopakana na njia muhimu za baharini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet