Afukuzwa kazi, kisa anatumia muda mrefu akienda chooni
Eric Buyanza
March 21, 2024
Share :
Vyombo vya habari vya China viliripoti kisa cha ajabu cha mfanyakazi anayeitwa Wang ambaye alimshtaki mwajiri wake kwa kumuachisha kazi kwasababu ya kutumia muda mwingi chooni wakati wa saa za kazi.
Hata hivyo ilibainika Bwana Wang baada ya kufanyiwa upasuaji wa tatizo la haja kubwa, aliendelea kupata maumivu na usumbufu, hivyo alianza kutumia saa tatu hadi sita chooni kila siku.
Mwajiri huyo wa zamani wa Wang anadai kwamba katika kipindi cha siku 10, alichukua jumla ya mapumziko 22 kwa kwenda chooni, ambayo yalichukua kati ya dakika 47 hadi masaa 6.
Mnamo Oktoba 2015, Bw. Wang alitaka kurudishwa kazini, na pande hizo mbili ziliingia kwenye vita vya kisheria vilivyomalizika mwaka jana, wakati mahakama kuu ya jiji la Tianjin ilipotoa maamuzi kwamba mapumziko ya chooni ya Bwana Wang hayakuwa sahihi kwa mazingira ya kawaida ya kikazi.
Wang hakurudishiwa kazi yake.