Afungiwa miezo 6 baada ya kumpa kipigo refa
Sisti Herman
February 4, 2024
Share :
Mchezaji wa timu ya Police FC Rwanda beki Ndizeye Samuel amesimamishwa kujihusisha na soka kwa muda wa miezi sita baada ya kumpiga kichwa mwamuzi.
Katika wiki ya 16 ya Ligi Kuu Rwanda, timu ya Police FC ambayo ndiyo ilikuwa mwenyeji wa mchezo iliweza kupoteza kwa kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Sunrise FC.
Ndizeye Samuel mchezaji wa kimataifa wa Burundi alimpiga mwamuzi Nsabimana Patrick ambaye alikuwa kibendera namba mbili baada ya kutoridhishwa na maamuzi yake.
Tukio hilo ni baada ya kukataa bao ambalo lilikuwa limefungwa na Nahoha wa Police FC Nshuti Dominique Savio ikidaiwa kuwa alikuwa ameotea.
Hata hivyo Police FC imekataa rufaa kuhusiana na adhabu aliyopewa mchezaji huyo.