Afunguliwa mashitaka kwa kupaka nywele zake rangi ya 'Njano na Bluu'
Eric Buyanza
May 2, 2024
Share :
Kijana mmoja wa jijini Moscow nchini Urusi, hivi majuzi alipigwa faini na kufunguliwa mashtaka na polisi kwa kupaka nywele zake rangi ya 'Njano na bluu', rangi ambazo zinapatikana kwenye bendera ya Ukraine.
Usiku wa Aprili 27 akiwa anatoka kazini kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Stanislav Netesov alishambuliwa na watu wasiojulikana kwenye kituo cha basi katikati ya mji wa Moscow.
Watu hao walimng'oa jino kutokana na kipigo pamoja na kumpora simu yake, hata hivyo cha kushangaza kesho yake alipokwenda kuripoti uhalifu aliofanyiwa polisi walimbadilikia na yeye ndiye akageuka kuwa mhalifu kutokana na rangi ya nywele zake.
Polisi walizichukulia nyewele za Netesov kama ishara ya kuiunga mkono Ukraine, jambo ambalo ni kosa kwa jeshi la Urusi, ambalo linaadhibiwa kisheria.
Inaelezwa kuwa Mahakama za Urusi zinachukulia taarifa zozote za kupinga vita kuwa ni uhalifu na kulidharau Jeshi la nchi hiyo, na adhabu yake ni faini ya dola 543 na kifungo cha hadi miaka mitano jela kwa makosa yanayojirudia.