Afya ya Celine Dion yawaumiza Mashabiki azidi kudhoofika.
Joyce Shedrack
July 2, 2024
Share :
Malkia wa Muziki kutoka Nchini Canada, Celine Dion ameweka wazi hali yake ya Afya na kuonyesha jinsi ugonjwa nadra wa kingamwili unavyoathiri mfumo wa neva "Stiff Person Syndrome" (SPS) kiasi cha kumnyima uwezo wa kutembea,kuimba, na kudhoofika mwili.
Celine ameweka wazi hilo kupitia Documentary yake mpya ya "I Am: Celine Dion" inaonyesha jinsi maisha yalivyobadilika tangu agundulike kuwa na ugonjwa huo ambao husababisha misuli na ngozi kukaza bila kudhibitiwa na kupata kifafa cha kutisha kinachodumu kwa muda mfupi.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2022 Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 56 aliweka wazi kwamba anapambana na matatizo ya afya, ikiwemo mishtuko ya misuli na kukakamaa na kugundulika rasmi kuwa na ugonjwa huo nadra ambao huwakumba watu wachache Duniani.