pmbet

Ahadi aliyoitoa Bashungwa, Imemzalia zawadi kutoka Kilwa

Eric Buyanza

May 29, 2024
Share :

Waziri wa Ujenzi Mh. Innocent Bashungwa amekabidhiwa zawadi ya jogoo na wananchi wa Kilwa kwa juhudi kubwa za Wizara yake kurejesha mawasiliano ya Barabara katika eneo la Tingi – Kipatimo, na Barabara Kuu inayounganisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara.

Zawadi hiyo imetolewa na Mzee Kimbwembwe kutoka Kijiji cha Somanga, ikiwa ni saa chache kabla ya Bashungwa kuwasilisha bajeti yake bungeni kwa mwaka 2024/25.

“Na wewe Bashungwa (Waziri wa Ujenzi) kwa kauli moja sisi wananchi wa Kilwa tumekuletea zawadi hii kutokana na kazi kubwa uliyoifanya kwa kurudisha mawasiliano ndani ya saa 72 kama ulivyoahidi,” amesema.

Mzee huyo amesema kilichowafurahisha wananchi wa huko ni kitendo cha Waziri kukaa huko kwa siku tano akishughulikia urejeshwaji wa miundombinu iliyokatika kwa sababu ya mvua jambo ambalo wao wameona aliwajali sana.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet