pmbet

Ahmed Ally aingilia sakata la Mzize "Ni unyonyaji".

Joyce Shedrack

August 11, 2025
Share :

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya  Simba Ahmed Ally ameingilia kati sakata la mchezaji wa Yanga Clement Mzize baada ya tetesi kuwa wananchi wameikataa ofa ya kumnunua iliyofika mezani kwao kutoka Nchini Tunisia.

Ahmed Ally ameandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram akiweka wazi kuwa kumzuia mtu asitimize malengo yake ni unyonyaji.

 

“Ni wakati sahihi mimi kuingilia kati sakata la Sheikh Walid, kuhakikisha kijana anaenda kutimiza ndoto yake ya kucheza Nje ya Nchi.Naingilia kati kuhakikisha kijana anauzwa kwa thamani yake halisi na sio Bei za kukurupuka ili kukwamisha Biashara makusudi”

“Haiwezekani kila mchezaji akitaka kuondoka kwenu ianze vita, Kwa Mayele tulijua bahati mbaya kwa Feisali tukasema haitojirudia tena na sasa kwa Walid hii haikubaliki”

“Kuzuia mtu asitimize malengo yake ni unyonyaji na unapotaja Bei isiyoendana na uhalisia ni lugha iliyojificha ya kumwambia mtu siuzii bidhaa hii Hili siwezi kulifumbia macho, Tulimnusuru Mayele, tukamkomboa Fei na sasa ni zamu ya Walid”

“Kwako Walid wewe endelea kuipigania Tanzania, sisi tutapambana nao na mwisho wa siku tutakukabidhi ushindi Insha Allah”Ameandika Ahmed Ally.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet