Ahmed Ally alia na viingilio vya mchezo wao dhidi ya Azam FC.
Joyce Shedrack
April 4, 2026
Share :
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema klabu hiyo inapinga vikali viingilio hivyo akidai ni mpango wa kuwanyong’oshesha mashabiki wa klabu hiyo na kuiomba Bodi ya Ligi kuwajali mashabiki wa mpira huku.
Ahmed amesema licha ya Azam FC kuwa wenyeji wa mchezo huo, lakini kiingilio cha chini cha Tsh elfu 15 hakijawahi kuwekwa katika mpira wetu.
“Sisi tunaweza kuwaambia mashabiki wetu tu wasiende uwanjani na Azam FC tunajua hawana mashabiki halafu tuone mechi ya pili kwa ukubwa inachezwa majukwani hakuna watu.? Wao Azam FC watajisikiaje” amesema Ahmed Ally.
Viingilio ni kwa tiketi za VIP B Tsh 25,000 na Tsh 30,000 kwa tiketi za VIP A na Mzunguko 15000 huku mashabiki wa Soka wakionesha kushangazwa na kiwango kiwango hicho cha viingilio mbali na gharama kubwa ya usafiri wa kwenda Chamazi, Mbagala.





