pmbet

Ahmed Ally atoa neno baada ya kipigo cha Stade Malien.

Joyce Shedrack

December 1, 2025
Share :

Baada ya kichapo cha mabao 2-1 ilichokipata Simba SC dhidi ya Stade Malien ya Mali, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ametoa neno.

Ahmed ambaye hajasafiri na timu kwenda nchini Mali kwa ajili ya mchezo huo ameandika kuwa “ Mechi yetu ya 3 ya hatua ya Makundi tutacheza January 21 2026 dhidi ya Esperance ugenini.

“Kutoka leo hadi January 21 ni siku zaidi ya 50 katika siku hizo kikosi chetu kitafanyiwa mabadiliko makubwa ya kiufundi na itakapobidi kuongeza nguvu kwenye dirisha dogo tutafanya hivyo, na tunaamini mabadiliko hayo yataturejesha kwenye makali yetu.

“ Umefika ule wakati wa Simba yetu kuonesha maajabu yake na kuwashangaza watu kwa comeback yetu kwa sasa kikosi kinarejea na moja kwa moja tunaanza maandalizi ya michezo yetu ya Ligi kuu.

Ahmed aliendelea kuandika kuwa “ Tukumbuke kuwa katika Ligi tuna mwenendo mzuri hivyo tunapaswa kuwekeza nguvu kubwa tusiteleze kwa sasa kila Mwana Simba aelekeze nguvu na akili katika mchezo wetu dhidi ya Mbeya City na Azam Fc”.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet