Ahmed Ally awatuliza mashabiki Seleman Mwalimu kutua Simba.
Joyce Shedrack
August 11, 2026
Share :
Semaji la Mnyama @ahmedally_ ameandika ujumbe wake wa kwanza baada ya Selemani Mwalimu kutambulishwa Yanga.

"Wengi tumeingia kwenye taharuki baada ya kuona aliyekua mshambuliaji wetu kutambulishwa klabu nyingine"
"Kwanza niwape pole Wana Simba kwa taharuki hii"
"Sipo hapa kujielezea nini kimetokea, Kitu muhimu zaidi kwa sasa tuwekeze nguvu kwenye mchezo wetu wa kesho wa Ngao ya Jamii"
"Hakuna tunachokihitaji zaidi ya ushindi, kwa misimu miwili tumeikosa Ngao ya Jamii, Huu ndio wakati sahihi wa kuchukua Taji hili Insha Allah"
"Akili yetu, fikra zetu, mawazo yetu na nguvu zetu tuzielekeze Amaan Stadium, Safati hii tunatakiwa kuufungua msimu kwa Ubingwa wa Ngao"
"Tumerithishwa kuipenda Simba yetu hivyo tuendelee kuipigania kesho tupate furaha ya wote"Ameandika @ahmedally_ .





