Ahmed Ally azinduka, awatia moyo mashabiki
Sisti Herman
April 22, 2024
Share :
Siku 1 baada ya kipigo cha pili mfululizo kutoka kwa watani zao Yanga, Meneja wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameibuka kuwatia moyo mashabiki wa timu hiyo kama ilivyo kawaida yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ahmed ameandika;
"Dhahabu hupitishwa kwenye moto mkali ili ipate thamani na iwe bora"
"Licha ya kuwa huteseka inapopita kwenye moto huo lakini mwishoe hubaki safi, bora na thamani yake huongezeka maradufu"
"Wana Simba tuvumilie kupita kwenye moto huu mkali ili tuwe bora na hadhi yetu irejee"
"Najua maumivu ni makubwa kwa kua moto mkali lakini hatuna budi kuvumilia kwani ndio njia pekee ya kurudi kwenye thamani yetu"
Alimaliza kuandika Ahmed, Simba ilipoteza 2-0.