Ahukumiwa jela miaka sita kwa kumtusi Rais.
Joyce Shedrack
July 11, 2024
Share :
Mahakama nchini Uganda imemhukumu Edward Awebwa (24) kifungo cha miaka sita jela kwa kosa la kumtusi Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni na familia yake kupitia video aliyoichapisha kwenye mtandao wa TikTok.
Kijana huyo alishtakiwa hivi karibuni kwa matamshi ya chuki na kueneza taarifa za kupotosha na zenye nia mbaya juu ya Rais Museveni, Mke wa Rais Janet Museveni na mwanawe Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni Mkuu wa majeshi.
Licha ya kijana huyo kukiri kuwa na hatia na kuomba msamaha hakimu kiongozi Stella Maris Amabilis alisema kijana huyo hakuonekana kujutia kitendo chake na maneno yaliyotumiwa kwenye video hiyo yalikuwa machafu sana hivyo mshtakiwa anastahili adhabu ambayo itamwezesha kujifunza kuheshimu utu wa Rais na familia yake.
Abebwa amehukumiwa kifungo cha miaka sita kutokana na mashtaka manne yaliyokuwa yanamkabili.