Ahukumiwa kifo kwa kumuua shangazi yake, kisa alimnyima Baiskeli
Eric Buyanza
April 18, 2024
Share :
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imemuhukumu mkazi wa Mwigumbi, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Alex Masanja kunyongwa hadi kufa, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua shangazi yake Merisiana Malisa, mkazi wa kijiji cha Masagara wilayani humo.
Imedaiwa mahakamani kuwa Alex Masanja, alifanya tukio hilo kwa kukusudia usiku wa tarehe 16/2/2023 majira ya usiku wakati shangazi yake akiwa amelala, ndipo alipommvamia na kumpiga kwa kitu kizito kichwani na kusababisha kifo chake na baada ya hapo aliiba baiskeli ambayo aliiuza siku iliyofuata pamoja na simu na kutoroka kwenda kujificha mkoani Tabora.
Taarifa zinasema Alex alitenda tukio hilo baada ya kukatazwa kutumia baiskeli ya marehemu, kwa kuwa amekuwa akiichukua bila ruhusa na kuirudisha usiku wa manane.