pmbet

Ahukumiwa maisha jela kwa kulawiti watoto wawili

Sisti Herman

August 7, 2025
Share :

 

Mahakama ya Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza, imemhukumu Isack Marco Masheku (33), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Malya, kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwalawiti watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 7 na 9 (majina yamehifadhiwa kwa sababu za kisheria).

Hukumu hiyo imesomwa jana, Agosti 5, 2025, na Hakimu Mkazi Mhe. John Jagadi, ambapo mshtakiwa alipatikana na hatia kwa makosa mawili ya kulawiti, kinyume na kifungu cha 154(1)(a) na (2) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya 2022.

Kwa mara ya kwanza Masheku alifikishwa mahakamani Julai 23, 2025, katika kesi ya jinai namba 17942/2025, ambapo ilidaiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti mwezi Mei 2025, katika kijiji hicho hicho.

Katika utetezi wake, mshtakiwa aliiambia Mahakama kuwa alikosa fedha za kuwalipa wanawake wanaojiuza, hivyo akachukua uamuzi wa kuwalawiti watoto hao kwa kuwa hawakuhitaji malipo. Kauli hiyo ilipingwa vikali na Wakili wa Serikali, Juma Kiparo, aliyesisitiza kuwa kitendo hicho ni cha kikatili na kimewaathiri watoto hao kimwili na kisaikolojia.

Wakili Kiparo aliomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine na kusaidia kukomesha vitendo vya ukatili wa kingono dhidi ya watoto vinavyozidi kushamiri katika jamii.

Akitoa hukumu, Jagadi alisema Mahakama haina chaguo lingine zaidi ya kifungo cha maisha, kama inavyoelekezwa na sheria, na akaamuru mshtakiwa kutumikia kifungo cha maisha gerezani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet