Aibu, Bunge lakatiwa umeme!
Eric Buyanza
March 2, 2024
Share :
Shirika la usambazaji umeme la nchini Ghana imelikatia umeme Bunge la nchi hiyo kama hatua ya kulishinikiza kulipa deni la dola milioni 1.8 inazodaiwa na shirika hilo.
Tukio hilo lililotokea Alhamisi wiki hii lilivuruga mjadala bungeni, Mkurugenzi wa mawasiliano wa shirika hilo, William Boateng, alithibitishia shirika la habari la Reuters kuwa iliamua kufanya hivyo baada ya Bunge kushindwa kutimiza ahadi ya kulipa deni lake.
Hata hivyo, umeme ulirudishwa muda mfupi baadaye baada ya bunge hilo kulipa dola milioni moja na kuahidi kulipa fedha nyingine haraka iwezekanavyo.