Aibu, umeme wakatika Rais akihutubia, mawaziri tumbo joto!
Eric Buyanza
February 26, 2024
Share :
Shida ya umeme kukatika mara kwa mara imekuwa shida na kero kubwa kwa nchi zetu za kiafrika.
Hivi majuzi ilikuwa tafrani nchini Kenya pale umeme ulipokatika wakati Rais William Ruto akiwa ameshika microphone juu ya meza kuu akiwahutubia wakenya.
Hali hiyo iliwaweka roho juu baadhi ya mawaziri waliokuwa eneo la tukio na wasijue la kufanya.
Kwenye video iliyorekodiwa na televisheni ya NTV ya nchini humo, anaonekana Rais Ruto akisema "sababu iliyofanya niwateue ni kwa sababu nilijua mna uwezo wa kufanya kazi mnayofanya”.....mara ghafla paaa umeme ukakata na eneo hilo likagubikwa na ukimya wa ajabu.
Kwa mbaaali akaonekana Rais Ruto akigonga gonga kipaza sauti kama vile anafanya majaribio ya sauti.
Ilichukua dk kadhaa umeme kurejea lakini ulikatika tena kwa mara ya pili rais akiwa bado hajamaliza hotuba yake...jambo lililosabisha amalizie hotuba kimya kimya kwenye giza.
TAIFALEO