pmbet

AICC kujenga ukumbi mkubwa wa mikutano wa kimataifa Arusha

Sisti Herman

March 13, 2025
Share :

 

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimesaini mkataba wa ushirikiano na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha mikutano cha kimataifa chenye thamani ya zaidi ya Sh385 bilioni.

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mlima Kilimanjaro (MKICC) kinachotarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili, huku kituo hicho kikitarajiwa kufunguliwa mwaka 2027, kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati.

Mkataba huo ulitiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Bi Christine Mwakatobe, na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw Abdul Razzaq Badru, Jumapili Machi 09, 2025.

Kituo hicho kitakuwa na ukumbi mkubwa wa kuchukua watu zaidi ya 5,000, hoteli ya nyota tano yenye vyumba 500, vyumba 10 vya rais, eneo la biashara la mita za mraba 20,000, maegesho ya magari 2,000, na sehemu ya kutua kwa helikopta.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameeleza kuwa mkoa huo unaitangaza vyema MKICC ili kuvutia mikutano ya kimataifa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet