Aina ya vyakula tunavyokula huchangia kunuka kwa kwapa
Eric Buyanza
April 8, 2026
Share :

Vyakula vyenye sukari nyingi, vyenye mafuta mengi, au ulaji wa nyama mara kwa mara vinaweza kuongeza harufu mbaya ya mwili. Utafiti wa mwaka 2025 wa Jarida la Journal of Clinical Medicine la Uswisi limetaja uhusiano kati ya tabia ya lishe na harufu ya jasho kali au kikwapa inavyosababishwa na ulaji na hali ya umeng'enyaji wa chakula kwenye mfumo wa binaadamu.
Harufu kali ya jasho la mwili, hasa kwenye maeneo kama kwapani, ni matokeo ya bakteria aina molekuli za jasho na kuachilia vitu vinavyonuka.
Wapo watu ambao suala la kuwa na jasho kali au kunuka kikwapa hulichukulia kama jambo la aibu, hivyo huamua kutumia njia mbalimbali za asili ili kujisitiri.
Ulaji wa chakula ni wazi kwamba kuna una uhusiano wa moja kwa moja wa kusababisha jasho kali au kikwapa hii husababishwa na baadhi ya vyakula vyenye viungo vikali kama vitunguu saumu na vitunguu maji ambavyo vinajulikana kuwa na sulfur nyingi, ambayo huingia ndani ya mwili na kutolewa kupitia jasho. Vyakula vyengine ni kama nyama nyekundu na vyakula vyenye sukari nyingi ikiwemo soda na pombe.
Godfrey Mwanyahi ni Daktari anasema suala la kunuka kikwapa,ni jambo linalosabishwa na ulaji wa chakula huku akiona kuwa hilo linaweza kuepukika.
Anasema sababu za kunuka kwa kikwapa ni nyingi, zikihusisha lishe, aina ya chakula kinacholiwa, mmeng'enyo wa chakula tumboni na bakteria wa utumbo na vyote hivi vinaweza kusababisha gesi zenye harufu isiyopendeza.
Aina ya matunda na mboga mboga ni baadhi ya suluhisho la kukata kabisa kunuka kikwapa. Matunda yenye maji mengi kama tikiti maji, miwa husaidia kuongeza unyevunyevu mwilini na kusafisha mfumo wa mmeng'enyo, hivyo kupunguza sumu zinazoweza kusababisha harufu mbaya.
Dkt Godfrey Mwanyahi anashauri kula vyakula kadhaa ili kupunguza jasho kali: " Vyakula vyenye ndimu ni miongoni mwa vyakula sahihi vinavyosaidia afya ya tumbo na kupunguza harufu mbaya ya kikwapa, kwani ndimu husaidia kusawazisha mmeng'enyo wa chakula na kuondoa baadhi ya gesi zisizo na harufu nzuri," alisisitiza Daktari huyo.
DW





