pmbet

Aina za Viungo kulingana na uwezo wao kiufundi

Sisti Herman

June 28, 2024
Share :

Katika kuangalia na kupima uwezo wa wachezaji uwanjani lazima maeneo makuu mawili yatumike kuwapima uwezo huo, uwezo wao kiufundi (technical ability) na uwezo wao wa kuelewa na kutimiza mbinu za makocha (tactical understanding ability)

 

Viungo wa kati wapo wa aina tofauti kama viungo wa kati wazuiaji ( defensive midfielder) viungo wa kati washambuliaji (Attacking Midfielder) viungo wa kati wanaoweza kusaidia timu kushambulia na kuzuia (box to box midfielder) lakini aina hizi zote zinaingia kwenye kuwajua wachezaji kwa jinsi wanavyotizima majukumu ya kimbinu uwanjani

 

Lakini linapokuja suala la uwezo wa kiufundi ndio tunang'amua kuwa je mchezaji huyu anafaa kucheza nafasi hii kulingana na uwezo wake kiufundi? na hapo ndipo nilipokuja na Somo la leo kwenye kuwajua viungo wa kati kulingana na uwezo wao kiufundi (technical ability) na aina nilizolenga ni hizi;

 

VIUNGO WENYE UWEZO WA KOKOTA MPIRA NDIO WATOE PASI (PROGRESSIVE BALL CARRIER)

 

Hawa ni aina ya viungo ambao wana uwezo mkubwa kiufundi kuweza kukokota mpira zaidi ya mita 5 ndio wapige pasi na mara nyingi kimbinu hupangwa kama viungo wa kati washambuliaji (kuanzia Box to box midfielder, Attacking midfielder hata wide midfielder)

 

Faida kubwa ya viungo wa aina hii ni kuwa wanaweza kuvunja mistari ya uzuiaji ya wapinzani kwa kukokota mpira ndipo wapige pasi kwani wanakua hawazuiliki kirahisi pale wanapokua kwenye shinikizo (press resistant) Pia husifika kuwa na mguso wa kwanza mzuri (first touch)

 

Athari kubwa ya viungo wa aina hii ni kuwa wanapopangwa kucheza kama viungo wazuiaji huweza kukokota mpira na kuondoka kwenye nafasi ambapo hushindwa kuiziba kwa wakati pale wanaposhambuliwa, pia wengi wao sio wazuiaji wazuri mfano Bernardo Silva, Martin Odergad, Kelvin De Bruyne, Andres Iniesta, Luca Modric nk

 

VIUNGO WENYE UWEZO WA KUPIGA PASI WAKIWA KWENYE NAFASI BILA KUHAMA MARA KWA MARA (PASSER)

 

Hawa ni viungo ambao wana uwezo mkubwa kiufundi kuweza kupiga pasi ndefu au fupi bila kuhama kwenye nafasi kwa kukokota sana mpira yaani ukimpa anaachia haraka

 

Faida kubwa ya viungo wa aina hii huweza kupiga pasi sahihi zinazoweza kuvunja mistari ya uzuiaji ya wapinzani bila kupotea pia huku wao wakiwa kwenye nafasi zao mfano Toni Kroos, Rodri, Xavi Hernandez, Joshua Kimmich, Kovacic, Tchoumeni na Sergio Busquet

 

Pia faida kubwa ni kuwa wengi wao huwa nguzo muhimu kulinda kwasababu huwa hawahami na kuacha nafasi kubwa mbele ya safu ya Mabeki wa timu zao

 

Athari kubwa ya viungo hawa ni kuwa kuna michezo ambayo timu itahitaji mtu anayeweza kukimbia na mpira umbali mrefu ili kuvunja mistari ya uzuiaji hasa wanapokua kwenye shinikizo halafu wao wakawa hawana uwezo hitajishi 

 

Pichani nikiwa na viungo wa timu ya taifa ya wanawake Tanzania "Twiga Stars" Diana Lucas Msewa anayecheza soka la kulipwa nchini Morocco kunako klabu ya AUSFAZ na Irene Kisisa "Rodrigo" anayecheza Yanga Princess ambao wote kwa pamoja kiufundi ni Progressive Ball Carriers 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet