pmbet

Aingia shule na bunduki ya mama yake na kuua mwalimu na wanafunzi 3

Eric Buyanza

October 16, 2026
Share :

Watu wanne, wakiwemo watoto watatu na mwalimu mmoja, wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kijana mwenye umri wa miaka 16 kuvamia Shule ya Msingi ya Silver Rail mjini Bend, Oregon, Alhamisi alasiri.


Kijana huyo mwenye silaha naye aliuawa kwa kupigwa risasi na mwananchi mmoja aliyekuwa karibu na eneo hilo kabla ya polisi kufika.

Polisi walipokea simu kutoka kwa mtu aliyekuwa kwenye gari akiripoti kuwa kuna mtu anafyatua risasi nje ya shule kwa kutumia bunduki ndefu.


Mkuu wa Polisi wa Bend, Mike Krantz, alieleza kuwa kijana huyo alilazimisha kuingia ndani ya jengo la shule kwa kupiga risasi milango iliyokuwa imefungwa. Mwananchi mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alimfuata mtuhumiwa huyo ndani ya shule na kumpiga risasi iliyomuua papo hapo.

 

Mamlaka zote zimebaini kuwa mshambuliaji alikuwa kijana wa miaka 16 mkazi wa eneo hilo, na alitumia bunduki ya aina ya shotgun iliyonunuliwa na mama yake. Polisi wakisaidiana na shirika la FBI wanaendelea kuchunguza chanzo na nia ya shambulio hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet