Aisha Masaka mchezaji bora wa kike tuzo za BMT
Sisti Herman
June 2, 2025
Share :
Nyota wa Brighton & Hove Albion Women na nyota wa Twiga Stars Aisha Masaka ameshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka wa kike kwa mwaka 2024.
Mshambuliaji huyo wa kandanda ametwaa tuzo hiyo akimshinda Mwanamasumbwi Rehema Abdallah na mchezaji wa gofu Madina Iddy.
Tuzo hizi zinatolewa usiku huu na Baraza la Michezo la Taifa 'NSCA 2024' katika ukumbi wa Super Dome-Masaki.