pmbet

Aishi miaka 50 akinywa maji tu!

Eric Buyanza

December 9, 2023
Share :

Wahenga walisema kuishi kwingi kuona mengi, maneno yao yanathibitishwa na kisa hiki cha ajabu huko nchini Vietnam.

Katika hali ya kushangaza, Bibi wa Ki-Vietnam hajakula chakula cha aina yoyote kwa miaka 50 zaidi ya maji na soda tu
 

Bibi huyo wa miaka 75 aliyefahamika kwa jina la Bui Thi Loi bado anaonekana mwenye nguvu na afya tele na hasumbuliwi na magonjwa ya aina yoyote na amekuwa akiendelea na shughuli zake za kutunza makaburi ya jeshi kama mfanya usafi.
 

Kwa mujibu wa Bibi huyo aliacha kusikia njaa baada ya kupigwa na radi, akisimulia kisa hicho Bibi Loi anasema, mwaka 1963 akiwa na wenzake walikuwa wakipanda mlima kwenda kuwasaidia wanajeshi waliojeruhiwa vitani na ndipo alipopigwa na radi na toka siku hiyo aliacha kusikia njaa na anasema anajisikia hovyo anaposikia harufu ya chakula.
 

Waandishi wa habari wanaomtembeleaga mara kwa mara Bibi huyu wanasema hukuta friji lake likiwa limejaa chupa za maji na soda tu.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet