Aishi siku 555 na moyo wa bandia kwenye begi la mgongoni
Eric Buyanza
February 26, 2024
Share :
Mwaka 2014 Stan Larkin aliishi kwa siku 555 bila moyo halisi, alibeba ‘moyo wa bandia’ kwenye kibegi cha mgongoni kwa masaa 24 na siku 7 za wiki kwa muda wa siku 555. Moyo huo wa bandia ulisukuma damu mwilini mwake na kumuweka hai katika siku zote hizo.
Stan akiwa na kibegi hicho, pia aliweza kucheza mchezo anaoupenda wa (mpira wa kikapu). Baadae alikuja kufanyiwa upandikizaji wa moyo baada ya kupatikana kwa moyo halisi kutoka kwa mfadhili (donor).
Kwenye mataifa ya wenzetu kuna benki za viungo (Organ Bank) ambapo watu hujitolea viungo vya vya miili yao kabla hawajafa na kuhifadhiwa hapo, na wengine hutoa maelekezo kuwa wakikaribia kufa basi kiungo chake flani kitolewe ili kisaidie watu wenye uhitaji.