Ajali ya ndege yaua 18, rubani peke yake ndiye aliyepona
Eric Buyanza
July 24, 2024
Share :
Takriban watu 18 wamefariki dunia baada ya ndege iliyokuwa na watu 19 kuanguka na kuwaka moto dakika chache baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tribhuvan nchini Nepal.
Rubani wa ndege hiyo ambaye ndiye pekee aliyenusurika katika ajali hiyo mbaya anapatiwa matibabu kwenye moja ya hospitali nchini humo.
Inaelezwa kuwa ndege hiyo ya kampuni ya Saurya Airlines ilikuwa ikifanyiwa majaribio, na ilikuwa imebeba wafanyakazi wa ndege pamoja na mafundi.