pmbet

Ajali ya 'Noah' yaua watu wanne Singida

Sisti Herman

June 21, 2024
Share :

Watu wanne wamepoteza maisha na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu katika Kijiji cha Nkwae mkoani Singida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Amon Kakwale amesema leo Juni 21, 2024 kuwai chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Noah aliyeshindwa kulimudu gari lake akiwa katika mwendokasi.

Kamanda Kakwale amesema miongoni mwa waliohusika kwenye ajali hiyo, yumo mhandisi wa halmashauri ya Hanang, Mwasaku Zabron (37) aliyekuwa anatoka mkoani Mwanza kwenda Katesh mkoani Manyara.

Amesema ajali hiyo ilitokea saa 3 usiku Juni 19, 2024 katika kijiji cha Nkwae, Kata ya Msisi mkoani Singida,, ikihusisha gari aina ya Noah ambalo lililogonga kwa nyuma gari aina ya Mercedes Benz, kisha nalo likagongwa kwa nyuma na gari Toyota Carina lililokuwa linaendeshwa na Mhandisi Mwasaku.

Kakwale amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Kidanga Ntandu ambaye ni dereva na mmiliki wa Noah hiyo, Ally Ibrahim (40), James Anthony (45) na mwanaume mmoja ambaye hajafahamika aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45, wote wakiwa ni wakazi wa mkoa wa Singida, ambao walikuwa abiria kwenye Noah.

Amesema miili ya marehemu ilipelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida ikisubiri kukabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi huku majeruhi wakiendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet