pmbet

Ajali yaua 9 Bagamoyo

Sisti Herman

March 11, 2024
Share :

Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari mawili wilayani Bagamoyo Mkoa Pwani jana Machi 10, 2024 jioni.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa dereva wa lori alikuwa anayapita magari yaliyokuwa mbele yake kwenye eneo lisiloruhusiwa, ndipo alipogongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Toyota Coaster.

"Ajali imetokea eneo la Kiromo Bagamoyo Mkoa wa Pwani na dereva wa lori aliyekuwa akitokea Bagamoyo kwenda Dar es Salaam alikuwa anayapita magari kwenye eneo lisiloruhusiwa, ndipo akagongana uso kwa uso na gari ya abiria aina ya Toyota Coaster iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo," amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema kuwa kati ya waliopoteza maisha, saba ni wanaume na wawili ni wanawake.

"Majeruhi watatu wamefikishwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya matibabu," amesema.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet