Ajali yaua watu 13 Kilwa
Sisti Herman
April 22, 2024
Share :
Watu 13 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili eneo la Somanga wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amesema leo Jumatatu Aprili 22 ,2024 kuwa, ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi Barabara Kuu ya Somanga-Nangurukuru baada ya gari ndogo ya abiria kugongana uso kwa uso na lori la mafuta
Majeruhi wote sita wamepelekwa katika Hosptali ya Tingi kwa ajili ya matibabu zaidi pamoja na miili 13 imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Hosptali ya Tingi iliyopo wilayani Kilwa, mkoani Lindi.