pmbet

Ajali yaua watu 7 na kujeruhi watu 32 Mwanga

Sisti Herman

April 3, 2025
Share :

 

Watu saba wamefariki dunia papo hapo huku wengine 32 wakijeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Mvungi, walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Kijiji cha Mamba, Kata ya Msangeni, Tarafa ya Ugweno, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Kamanda ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, ambapo amesema ajali hiyo imetokea leo Alhamisi saa moja asubuhi, Aprili 3, 2025 ambapo basi hilo lilikuwa likitoka Ugweno kwenda mkoani Dar es salaam.

Amesema waliofariki katika ajali hiyo ni wanawake watatu akiwemo mtoto mdogo na wanaume wanne.

Ajali hiyo imetokea ikiwa zimepita siku nne tangu itokee ajali nyingine Machi 30,2025 iliyoua watu saba kwa matukio mawili tofauti wilayani Same, ikiwemo iliyoua wanakwaya sita wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mmeni Chome, Dayosisi ya Pare iliyotokea katika milima ya Pare baada ya gari walikuwa wakisafiria kupinduka katika milima hiyo.

Akizungumzia tukio hilo la ajali, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo lilikuwa likijaribu kupishana na gari jingine na ndipo lilipoteleza kwenye tope na kupindika.

pmbet

pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League

pmbet
pmbet