pmbet

Ajifungia kichwa ili asiweze kuvuta fegi!

Eric Buyanza

January 6, 2024
Share :

Watu wengi wamejaribu kuacha kuvuta sigara kwa kutumia njia tofauti tofauti, wako waliofanikiwa na ambao hawakufanikiwa, lakini mwaka 2013 jamaa mmoja huko nchini uturuki alitoa kali ya mwaka baada ya kuamua kujijengea kitu kama uzio kwenye kichwa chake kama mbinu ya kuacha sigara.....na mkewe ndiye aliyekuwa akikaa na funguo na alikuwa akimfungulia  wakati wa kula tu.
 

Jamaa huyo aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Yucel alichukua hatua hiyo ili kutimiza azma yake ya kuachana na uvutaji wa sigara.

Yucel aliunda kichanja chenye waya za chuma, ili kuingiza kichwa chake na kufunga kwa kufuli mbili. Lengo hilo lilitokana na hatua mbaya aliyofikia ya kuvuta pakiti mbili za sigara kwa siku kwa zaidi ya miaka 20.
 

Yucel aliwakabidhi funguo za kichanja hicho mkewe na mwanae wa kike kila alipotaka kutoka nyumbani kila siku, ili asiweze kufungua pale anapopatwa na hamu ya kuvuta sigara.
 

Inaelezwa hatua hiyo ilikuja miezi michache baada ya kumpoteza baba yake kwa ugonjwa wa saratani ya mapafu, ambayo wataalamu walisema ilisababishwa na uvutaji wa sigara, Yucel aliona sio jambo zuri kuendelea kuvuta sigara katika maisha yake kwani anaiweka familia yake hatarini haswa baada ya kuona yaliyompata baba yake mzazi.
 

Yucel alivutiwa na wazo la kofia ngumu za kuendesha pikipiki (helmet) na kuamua kutengeneza kichanja cha waya za chuma ambao utamzuia kuwasha sigara hata akizidiwa na hamu.
 

Alipeleka wazo lake kwa mafundi chuma lakini walikataa kumtengenezea hivyo aliamua kufanya mwenyewe. Aliunganisha waya za kopa kwa kuziweka karibu karibu ili kuhakikusha sigara haiwezi kupenya na kisha kuongeza sehemu mbili za kubana kufuli.
 

Akamkabidhi ufunguo mmoja mkewe na mwingine bintiye, Ayse.
 

Japokuwa ilimlazimu kupambana kwa style hiyo, lakini pia Yucel  ilimlazimu kupambana na aibu ya kuvaa kidubwana hicho anapokuwa hadharani ili aweze kuishinda vita hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet