Ajifungua mapacha kwa saa 20
Sisti Herman
December 24, 2023
Share :
Mwanamke mmoja raia wa Marekani ambaye taarifa zake hivi karibuni zilienea katika mitandao ya kijamii kutokana na upekee wa maumbile ya uzazi ya kuwa na mifuko miwili ya uzazi [uterus] akiwa na ujauzito wa mapacha ambao wapo katika mifuko hiyo miwili, amejifungua watoto wawili ndani ya saa 20.
Kelsey Hatcher mwenye umri wa miaka 32, amejifungua mtoto wa kike siku ya Jumanne na mtoto mwingine wa kike siku ya Jumatano katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Alabama Birmingham (UAB).
Kwa maelezo ya kitaalamu mapacha hao hujulikana kama mapacha wasiofanana, japo kwa kawaida imezoeleka mapacha wa namna hiyo mimba hutungwa kutoka katika mayai mawili na mimba hiyo hukua katika mfuko mmoja wa uzazi [uterus], ila kwa mwanamke huyu mimba hiyo imetokana na mayai mawili na mimba hiyo kukaa katika mifuko miwili ya uzazi, jambo lilololeta utofauti na upekee katika maisha ya kawaida ya binadamu.