Ajifungua na kutupa mtoto kutoka ghorofani, akihofia kupoteza kazi
Eric Buyanza
July 9, 2024
Share :
Mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Katarina Jovanovic amehukumiwa kifungo cha miaka 7 jela baada ya kujifungua na kumtupa mtoto dirishani nje ya ghorofa analosihi huko Baden-Wuerttemberg nchini Ujerumani.
Mwanadada Jovanovic mwenye umri wa miaka 28 ni mwanasheria mkubwa tu na alijifungua kwa siri nyumbani kwake Septemba 12, 2023 mahakama ilisema.
Kitoto hicho kichanga kiliangukia pembeni ya barabara na kupasuka fuvu la kichwa kwa mujibu wa mashuhuda.
Waendesha mashtaka waliiambia mahakama jinsi Jovanovic alivyoamini kuwa kupata kwake mtoto kungemhatarishia kazi yake kama Afisa mkuu wa idara ya sheria wa kampuni kubwa ya utengenezaji wa magari ya Porsche.