pmbet

Ajitengenezea kichanja kichwani ili aache kuvuta 'fegi'

Eric Buyanza

May 11, 2026
Share :

Watu wengi wamejaribu kuacha kuvuta sigara, wako waliofanikiwa na ambao hawakufanikiwa.

 

Mwaka 2013 katika jitihada za kupambana na uraibu huo, jamaa mmoja huko nchini Uturuki aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Yucel alifanya uvumbuzi wa ajabu ambao ulizua gumzo kila kona ya dunia.

 

Yucel aliamua kujitengenezea kichanja cha kuvaa kichwani kwa lengo la kuishinda vita ya kuvuta sigara na funguo alimkabidhi mkewe ambaye alikuwa akimfungulia wakati wa kula pekee.

 

Mkewe aitwaye Kawthar alikuwa akimsumbua mumewe kwa miaka mingi ili aache kuvuta sigara bila mafanikio, ndipo Yucel alipoamua kujitengenezea kichanja cha waya za chuma ambacho anakuwa anaingiza kichwa na kufunga kwa kufuli mbili.

 

Lengo hilo lilitokana na hatua mbaya aliyofikia ya kuvuta pakiti mbili za sigara kwa siku kwa zaidi ya miongo miwili.

 

Mkewe Kawthar anasema hatua hiyo ya kuvaa kichanja ni ya kushangaza lakini kwa sababu mumewe ametia nia kutimiza lengo hilo, basi hana budi kumuunga mkono.

 

Miezi michache baada ya kumpoteza baba yake kwa ugonjwa wa saratani ya mapafu, ambayo wataalamu wanasema imesababishwa na kuvuta sigara, Yucel aliona sio jambo zuri kuendelea kuvuta sigara katika maisha yake kwani anaiweka familia yake hatarini haswa baada ya kuona yaliyompata baba yake mzazi.

 

Japokuwa ilimlazimu kupambana na uraibu huo unaosababishwa na hamu kubwa ya kuvuta sigara, Yucel pia ilimlazimu kupambana na aibu ya kuvaa kichanja hicho anapokuwa hadharani ili aweze kuishinda vita hiyo.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet