Ajizolea umaarufu kwa sababu ya kumnyonyesha mumewe
Eric Buyanza
May 15, 2024
Share :
Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja wa Florida nchini Marekani aliyefahamika kwa jina la Rachel Bailey, amekuwa gumzo baada ya kuweka wazi kuwa huwa anamnyonyesha mume wake.
Kwa sasa wanandoa hao wenye watoto watatu wanatarajia kuongeza mtoto wa nne ili tu waweze kupata maziwa ya kumnyonyesha mtoto pamoja na Baba.
Rachel na mume wake aitwae Alexander wamekuwa hawana raha tangu mtoto wao wa mwisho alipoacha kunyonya na hivyo Rachel kuacha kutoa maziwa.
"Nilikuwa nikinyonyesha mwanangu na mume wangu, na kisha siku moja mtoto wangu hakutaka tena kuendelea kunyonya maziwa yangu," Rachel aliiambia Caters News.
"Niliendelea kumnyonyesha Baba yake kwa muda wa wiki mbili, lakini ilikuwa ni kama mwili wangu ulitambua kwamba mwanangu hakuhitaji tena maziwa yangu na hivyo maziwa yalikata."
Kwa mujibu wa Rachel, tangu alipoweka wazi kuwa anamnyonyesha mumewe, amepata maombi yasiyo ya kawaida.
"Kuna wanaoniuliza kama naweza kuwauzia maziwa na wengine wamefika mbali wanataka kukutana na mimi ili niwanyonyeshe na wao,”.
"Tumepata maombi mengi kutoka kwa watu wakituomba tutengeneze video za jinsi ya kunyonyesha mtu mzima, lakini hatukuzingatia ingawa nina uhakika tungepata pesa nzuri."
Hata hivyo Rachel anasisitiza kwamba kumnyonyesha mume wake hajawahi kuliwaza kama jambo la kingono hata siku moja...bali analichukulia tendo hilo kama njia nzuri ya kuwaunganisha kama wanandoa.