pmbet

Akamatwa baada kujipodoa, ili amfanyie demu wake mtihani!

Eric Buyanza

January 16, 2024
Share :

Huko Punjab nchini India kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Angrez Singh amekamatwa baada ya kujifanya mwanamke ili aweze kumfanyia demu wake mtihani.

Kulingana na vyombo vya habari, mnamo Januari 7, 2024, mtihani kwa ajili ya wafanyakazi wa afya uliandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya cha Baba Farid.

Akiwa amevalia bangili nyekundu... amejipodoa kwa lipstck na kuvaa nguo za demu wake anayeitwa Paramjit Kaur, Angrez alitinga kwenye ukumbi wa kufanyia mtihani kwa ajili ya kuanza kazi aliyotumwa.

Hata hivyo baadhi ya wahadhiri wa chuo hicho waliingiwa na machale na kuanza kumfuatilia, ambapo baada ya kubananishwa alitoa vitambulisho feki ili kuthibitisha kuwa yeye ndiye Paramjit Kaur...jambo ambalo alifanikiwa.

Shughuli ilikuja pale alipotakiwa kuweka vidole kwenye mashine ya kutambua alama za vidole (fingerprints).....ambapo vidole vyake viligoma kumtambulisha kama Paramjit Kaur na ndipo polisi walipohusishwa kwa ajili ya hatua za kisheria. 

Pole sana Bwana Angrez.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet