Akamatwa kwa kubaka mtoto wa miaka 11, ajitetea alikuwa akimfundisha mapenzi
Eric Buyanza
February 13, 2024
Share :
Jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la, Terkimbi Sunday, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumbaka msichana wa miaka 11 huko Benue nchini Nigeria.
Mshukiwa huyo wa ubakaji alikamatwa Januari 25 na uchunguzi wa kimatibabu ulibaini kuwa mwathirika (binti) alikuwa na majeraha ya mwilini na kwenye sehemu yake ya siri.
Kwa mujibu wa polisi Bwana Sunday alikiri kufanya uhalifu huo na kujitetea kuwa binti huyo alimuomba amfundishe mapenzi.
Kwa mujibu wa polisi uchunguzi zaidi unaendelea kuhusu suala hilo na kwamba mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashitaka hivi karibuni.