Akamatwa uwanja wa ndege akiwa na nyoka 47 wenye sumu
Eric Buyanza
June 2, 2025
Share :
Mamlaka nchini India imemkamata mwanamume mmoja kwa kujaribu kuingiza nyoka wenye sumu ambao ni adimu kupatikana.
Raia huyo wa India, ambaye alikuwa akirejea kutoka Thailand, alizuiwa na maafisa wa forodha katika uwanja wa ndege mjini Mumbai siku ya Jumapili.
Maafisa walisema nyoka hao 47 wenye sumu kali, walikutwa wamefichwa kwenye begi la mtu huyo.
Mwanaume huyo ambaye hakutajwa jina yuko chini ya ulinzi na hajazungumza lolote tangu akamatwe.