Akata mkono wa mama yake, ili atumie vidole kuchukulia pesa benki
Eric Buyanza
April 24, 2024
Share :
Huko Brazil, kijana aliyefahamika kwa jina la Jose Natan Carvalho amemuua mama yake kwa kumkatakata kwa visu na kisha kumkata mkono ili atumie vidole vyake kuibia pesa kwenye akaunti ya benki.
Mwili wa Sandra Maria dos Santos Carvalho, mwenye umri wa miaka 58, ulikutwa nyumbani kwake katika jiji la Salvador, ukiwa umefunikwa kwa shuka na taulo.
Akiwa mahakamani Jose alikiri kumkata shingo mama yake na mkono wake kwa kisu na kudai alifanya hivyo kwa ajili ya tambiko la kichawi.
Alidai kuwa hapo awali mama yake alimfanyia yeye tambiko na kwamba aliamua kumuua ili kulipa kisasi.