Akutwa Hospitali panga linaning'inia kichwani huku akichezea simu
Eric Buyanza
July 10, 2026
Share :
Usiku wa tarehe 1 Mei 2026 katika eneo la Mankhurd huko Mumbai nchini India, kijana wa miaka 27 aliyefahamika kwa jina la Rohit Nagnath Pawar alikuwa amesimama karibu na banda la linalouza kuku wa kukaanga...dakika chache baadae akiwa hajui hili wale lile alivamiwa na vijana watatu ambao alikuwa na ugomvi nao siku za nyuma.
Mmoja wa vijana hao alimpiga kichwani akitumia panga kubwa lililopinda ambalo lilizama kwenye fuvu la kichwa cha Rohit na kisha vijana wale kikimbia.
Licha ya panga hilo kuwa limebaki likining'inia kichwani, Rohit hakupoteza fahamu. Rafiki yake alimbeba haraka kwenye pikipiki na kumuwahisha Hospitali.
Cha kushangaza Rohit alikuwa akitembea mwenyewe na alionekana amesemama mapokezi ya Hospitali bila kuonyesha dalili zozote za hofu au maumivu makali.
Wakati akisubiri madaktari wamhudumie, alionekana akiendelea kuchezea simu yake ya mkononi kwa utulivu mkubwa, jambo lililowaacha wagonjwa na wauguzi wengine wakiwa na mshangao mkubwa.
Rohit alifanyiwa upasuaji uliofanikiwa na panga hilo kutolewa, madaktari wakasema kuishi kwa kijana huyo ni muujiza mkubwa.






