Al Ahly haoo fainali, wawatoa TP Mazembe
Sisti Herman
April 27, 2024
Share :
Klabu ya Al Ahly ya Misri imetinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia ushindi wa jumla wa 3-0 dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo kwenye nusu fainali.
Al Ahly ambao mchezo wa awali ugenini DR Congo walilazimisha sare ya 0-0 jana magoli yao matatu yalifungwa na Abdelmonem dakika ya 68, Abou Ali dakika ya 84 na Tawfik dakika ya 90+13’
Al Ahly imeungana na Esperance Tunis kwenye fainali waliowaondosha Mamelodi Sundowns.