Al-Ahly hatuwaogopi tunawaheshimu, tuko tayari kupambana nao
Eric Buyanza
March 19, 2024
Share :
Kiungo wa Simba, Clatous Chama, amekiri kuwa mechi yao dhidi ya Al Ahly katika hatua ya robo fainali, itakuwa ngumu, lakini sasa ni muda wao wa kuandikia historia katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba inatarajiwa kuanzia nyumbani katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Al Ahly ya Misri unaotarajiwa kuchezwa Machi 29, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Chama amesema wanafahamu ubora wa Al Ahly, hivyo watacheza kwa kuwaheshimu kwa sababu wanahitaji kufanya vizuri ili kuandika historia mwaka huu.
"Malengo yetu ni kuona tunavuka robo fainali baada ya misimu minne kuishia hatua hii, Al Ahly si wageni kwetu, tumekutana nao mara nyingi, ni timu nzuri na bora lakini hatuwaogopi tunawaheshimu na tuko tayari kupambana,” amesema Chama.