pmbet

"Al Ahly wafe kwa Mkapa" - Ahmed Ally

Sisti Herman

March 13, 2024
Share :

Meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wanatumia michezo ya robo fainali minne ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika waliyofuzu miaka mitano iliyopita kama funzo ili kuweza kushinda mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Al Ahly hasa kwenye uwanja wa nyumbani.

 

“Katika Robo Fainali 4 za CAF tulizocheza hatukutumia ipasavyo mechi za nyumbani hivyo kazi ikawa ngumu mechi za ugenini”

“Safari hii mpango wetu ni kutumia kwa asilimia mia moja Uwanja wa Nyumbani yaani kumaliza mechi hapa Dar es Salaam”

“Mwana Simba popote ulipo anza kujiandaa na hii mechi, tunahitaji ushiriki wa kila Mwana Lunyasi ili tufanikiwe kumn’goa Al Ahly”

“Sio rahisi lakini inawezekana Insha Allah”

 

Hizi ni nukuu za msemaji huyo baada ya droo ya michuano hiyo kuwakutanisha na mabingwa wa kihistoria wa ligi ya mabingwa barani Afrika Al Ahly ya Misri mechi ambazo zitacheza mwishoni mwa mwezi huu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet