Al Ahly ya Misri hali tete huwenda wakaangukia shirikisho msimu ujao.
Joyce Shedrack
April 28, 2026
Share :
Klabu ya Al Ahly ya Misri ipo kwenye hatari ya kutokufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao wa 2026/27 baada ya mfululizo wa matokeo mabovu katika Ligi Kuu ya Misri.
Hali yao imekuwa mbaya zaidi kufuatia kichapo cha 3-0 walichopata dhidi ya Pyramids usku wa jana, tarehe 27 Aprili 2026, matokeo yaliyowaacha katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 44 huku Pyramids akiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya alama 47 na vinara Zamalek wakiwa na jumla ya alama 50.

Mchezo unaofuata dhidi ya vinara Zamalek kwenye dabi ya Cairo Jumamosi Mei 1, 2026,mchezo ambao endapo A Ahly wakipoteza, kuna uwezekano mkubwa wakakosa mashindano makubwa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003.
Ikumbukwe, ligi hiyo imebakiza michezo mitatu kwa timu zote ili kutamatika huku Al Ahly ikiwa imebakiza mechi dhidi ya Zamalek ugenini,dhidi ya ENPPI nyumbani Mei 5 na mechi ya kufunga msimu dhidi ya Al Masry ugenini Mei 15.
Al Ahly inahitaji ya ushindi wa mechi zao zote tatu huku wakiwaombea Pyramids na Zamalek wadondoshe alama kwenye michezo yao ili kuwashusha katika nafasi mbili za juu.





