Al Hilal inawataka Martinelli na Watkins wote kwa pamoja
Sisti Herman
August 23, 2026
Share :

Al Hilal inashughulikia kwa udi na uvumba mikataba miwili mikubwa ya kuwasajili mshambuliaji wa Aston Villa, Ollie Watkins, na winga wa Arsenal, Gabriel Martinelli.
Klabu hiyo ya Saudi Arabia inayofundishwa na Simone Inzaghi, imeweka kipaumbele katika kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili winga na mshambuliaji wa kati wa kiwango cha juu kabla ya dirisha la usajili la majira ya joto kufungwa.





