Al Hilal ya Ibenge kushiriki ligi kuu Tanzania bara
Sisti Herman
March 18, 2024
Share :
Klabu ya Al Hilal ya Sudan imewasilisha barua kwa mashirikisho ya soka ya nchi mbalimbali ikiwepo Tanzania kuomba kushiriki ligi kwaajili ya kuwa kwenye ushindani.
Hilo linakuja kipindi hichi baada ya ligi ya Sudan kusimama kwasababu za kiusalama baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe huku Hilal wakihitaji mechi za ushindani kwaajili ya kuwa timamu kwaajili ya hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa.
Moja kati ya mashirikisho yaliyopokea barua hizo ni pamoja na shirikisho la soka Tanzania (TFF) ambapo kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo barani Afrika Micky Jr, TFF imerdhia ombi hilo na kwasasa wapo kwenye hatua za mwisho za kikanuni kuangalia kama inawezekana kwa vigogo hao wa soka ukanda wa CECAFA kuja kushiriki ligi kuu Tanzania bara na kama kanuni zitaruhusu basi tutawashuhudia Al Hilal nchini.
Pia moja kati ya sababu zinazoweza kusaidia hilo kupita ni uhusiano mzuri kati ya Al Hilal na TFF pamoja na klabu kubwa za Tanzania yaani Simba na Yanga.