Al Hilal yampa Mo Salah ofa nono
Sisti Herman
December 15, 2025
Share :

Al Hilal wameripotiwa kumpa ofa nzuri Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 33 kama njia ya kumshawishi kuondoka Liverpool mwezi Januari kwa mkataba mkubwa wa miaka 3, huku vilabu vingine vya Saudi pia vinavutiwa naye.
Liverpool wanaweza kukubali ofa hiyo kutokana mgogoro wa wiki iliyopita kati ya mchezaji na timu, huku wakimtaja Antoine Semenyo kama mrithi wake.
Ikiwa Mmisri huyo atahamia Al Hilal ataungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool, Darwin Nunez.





