Al-Ittihad waandaa dau la Pauni milioni 25 kwa ajili ya Ederson
Eric Buyanza
May 27, 2024
Share :
Kipa wa Manchester City, Ederson anafukuziwa kwa udi na uvumba na Klabu ya Al-Ittihad kutoka Ligi Kuu ya Saudia.
Ederson mmoja wa makipa bora barani Ulaya bado ana miaka miwili kwenye mkataba wake na Man City, lakini taarifa zinaeleza kuwa Al-Ittihad wako tayari kuweka mezani pauni milioni 25 kama ofa ya awali kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 30.
Al-Ittihad imekuwa ikimtaka mchezaji huyo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.