pmbet

Al-Shabaab waishambulia hoteli mjini Mogadishu

Eric Buyanza

March 15, 2024
Share :

Wanamgambo wa Al-Shabaab wameishambulia hoteli moja maarufu iliyoko karibu na makazi ya rais mjini Mogadishu jana Alhamisi.
 

Mashuhuda wamesema tukio hilo lilitokea  majira ya saa tatu usiku kwa majira ya Somalia baada ya watu wenye silaha kuivamia hoteli hiyo ya SYL huku wakifyatua risasi.
 

Haikujulikana mara moja kama kulikuwa na vifo ama majeruhi na baadhi ya mashuhuda walisema polisi walifika muda mfupi baada ya uvamizi huo.
 

Al-Shabaab wanaofungamana na kundi la kigaidi la al-Qaeda wamekuwa wakifanya uasi dhidi ya serikali ya shirikisho inayotambuliwa kimataifa kwa zaidi ya miaka 16 na mara nyingi wamekuwa wakilenga hoteli ambazo hutembelewa na maafisa wa ngazi za juu wa Somalia na wa kigeni.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet