pmbet

Albamu ya Tyla yakimbiza Spotify

Sisti Herman

June 4, 2024
Share :

Mwanamuziki kutoka South Africa ambaye alijulikana zaidi kupitia wimbo wake wa ‘Water’ Tyla ameendelea kufanya vizuri kupitia ngoma zake, hii ni baada ya albumu yake iitwayo ‘Tyla’ kufikisha zaidi ya wasikilizaji (streams) bilioni moja katika mtandao wa Spotify.

Albumu hiyo yenye ngoma 14 akiwashirikisha wasanii kama Gunna, Tems, TravisScott na wengineo iliachiwa rasmi Machi 22, 2024 huku ikichukua miezi miwili tu kufikisha wasikilizaji bilioni 1.

Haya siyo mafanikio ya kwanza kwa Album hiyo kwani imewahi kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya ‘Billboard World Album Chart’ wiki chache tangu kuachiwa kwake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet