Album ya Nick Minaj yawa gumzo ulimwenguni!
Eric Buyanza
December 8, 2023
Share :
Ikiwa ni masaa machache yamepita tangu rapa kutoka nchini Marekani Nick Minaj kuachia albam yake mpya ya ‘Pink Friday 2’ sasa albam hiyo inaongoza kusikilizwa na kuangaliwa kwenye majukwaa yote ya muziki duniani.
Vyanzo mbalimbali vya habari vinaeleza kuwa albam hiyo kwa sasa imekuwa kama wimbo wa taifa kutokana na kufuatiliwa kwake kila kona.
‘Pink Friday 2’ ni albam yenye nyimbo 22, ikishirikisha baadhi ya wasanii wakubwa duniani kama Drake, J.cole na wengineo.