Alex Msama atupwa rumande kwa tuhuma za kutapeli viwanja
Eric Buyanza
April 20, 2024
Share :
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Slaa amemkabidhi kwa jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama kwa uchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili za kujipatia fedha kwa kuuza viwanja bila kuwapatia wahusika kwa zaidi ya miaka 15.
Waziri silaa ametoa maelekezo hayo ya kumkamata na kumuweka chini ya ulinzi katika Ofisi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi zilizopo mkoani Dar es salaam wakati alipomuita kuja kujibu tuhuma zinazomkabili kutoka kwa wananchi mbalimbali.